IPOA: UHUNI UNAHITAJI KUKOMESHWA
Kamishna wa Mamlaka Huru ya Kusimamia Utendakazi wa Polisi (IPOA), KenWilliams Nyakomita, amesema kuwa uhuni si changamoto ya kawaida ya kuvuruga utulivu wa umma bali ni suala linalohitaji kushughulikiwa kwa umakini.
Nyakomita amesema kuna dalili kwamba baadhi ya viongozi na watu wenye ushawishi wanatumia neno uhuni kuficha au kuhalalisha shughuli za makundi ya uhalifu ambayo tayari yamepigwa marufuku na serikali.
Amesisitiza kuwa ni muhimu vyombo vya usalama na wadau wengine kushirikiana kubaini na kukabiliana na makundi hayo ili kulinda usalama wa wananchi na kuimarisha utawala wa sheria.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































