#Local News

WAKULIMA WA MIWA  KERICHO WAPINGA MSWADA WA KUHAMISHA USIMAMIZI WA USHURU WA MIWA

Wakulima wa miwa wamepinga pendekezo la serikali la kuhamisha usimamizi wa ushuru wa zao hilo kutoka Kenya Sugar Board kwenda kwa taasisi nyingine mpya.

Wakizungumza katika eneo la Kipsige, Kaunti ya Kericho, wakulima hao walisema hatua hiyo huenda ikadhoofisha mageuzi yaliyofanywa hivi karibuni na kuathiri maendeleo yaliyopatikana katika sekta ya miwa.

Wameitaka serikali kuendelea kuimarisha mfumo uliopo badala ya kuanzisha taasisi mpya, wakisema mabadiliko hayo yanaweza kuleta mkanganyiko na kuathiri ustawi wa wakulima wa miwa.

Imetayarishwa na Hilda Ajema

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *