OKOTH OBADO APATIKANA NA HATIA YA MAUAJI
Aliyekuwa Gavana wa Okoth Obado pamoja na washtakiwa wenzake, Michael Oyamo na Caspal Obiero, wamepatikana na hatia ya kumuua mwanafunzi wa chuo kikuu, Sharon Otieno.
Uamuzi huo unahitimisha moja ya kesi zilizovuta hisia za wengi nchini kuhusu mauaji ya Sharon Otieno.
Akitoa hukumu hiyo Alhamisi, mahakama ilisema ushahidi uliowasilishwa na upande wa mashtaka uliwaunganisha Obado, Oyamo na Obiero na mauaji hayo, na hivyo kuwapatia hatia.
Imetayarishwa na Hilda Ajema
English 































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































