#Local News

MURKOMEN: DCI INACHUNGUZA MASHAMBULIZI YA OL KALOU

Waziri wa usalama wa ndani Kipchumba Murkomen amesema Idara ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) imeanzisha uchunguzi kuhusu watu wanaodaiwa kuwashambulia wapigakura na wanahabari wakati wa uchaguzi mdogo wa Ol Kalou.

Murkomen amesema wote watakaobainika kuhusika na matukio hayo watachukuliwa hatua kali za kisheria, akionya wanasiasa dhidi ya kuajiri wahuni kuvuruga shughuli za kisiasa.

Aidha, amesisitiza kuwa si wahusika pekee watakaokamatwa, bali pia wale watakaobainika kufadhili au kupanga mashambulizi hayo watafikishwa mbele ya sheria.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *