WATUMISHI WA UMMA WAKATAA MAPITIO YA MISHAHARA
Muungano wa Watumishi wa Umma nchini umekataa mapitio ya hivi karibuni ya mishahara yaliyotangazwa na serikali, ukisema ongezeko hilo ni la kawaida la kila mwaka na si nyongeza halisi ya mishahara.
Viongozi wa muungano huo wakiongozwa na Katibu Mkuu Lawrence Ochieng wamedai kuwa Tume ya Mishahara na Marupurupu (SRC) haikuzingatia mapendekezo yao yaliyolenga kukabiliana na gharama ya juu ya maisha.
Muungano huo umeipa SRC pamoja na Wizara ya Utumishi wa Umma muda wa siku 14 kusitisha utekelezaji wa mapitio hayo na kurejea kwenye mazungumzo, ukionya kuwa usipotekelezwa utaandaa mgomo wa kitaifa.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































