RIGATHI AELEZA IMANI YAKE YA KUSHIRIKI URAIS MWAKA UJAO
Aliyekuwa Naibu Rais Rigathi Gachagua amesema ana mpango mbadala iwapo atazuiwa kugombea urais katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2027.
Gachagua amesema kuwa ana matumaini kuwa kesi inayomkabili mahakamani itatolewa huku akifichua kuwa anatambua kundi la viongozi vijana walio tayari kuendeleza azma ya eneo la Mlima Kenya ya kutoa mgombea wa urais huku akipuuza madai ya changamoto za kisheria zinazomkabili zinaweza kuliacha eneo la Mlima Kenya bila mgombea wa kiti cha urais.
Imetayarishwa na Hilda Ajema
English 































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































