#Football #Sports

CASEMIRO AJIUNGA NA INTER MIAMI

Klabu ya Inter Miami imetangaza kumsajili kiungo nyota wa Brazil Casemiro baada ya kuondoka Manchester United kufuatia kumalizika kwa mkataba wake.

Casemiro mwenye umri wa miaka 34, ambaye ameichezea Brazil mechi 91 na kutwaa mataji matano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya akiwa na Real Madrid, sasa ataungana na Lionel Messi na Rodrigo De Paul katika kikosi cha Inter Miami.

Hata hivyo, Ligi Kuu ya Marekani (MLS) imesema imeanzisha uchunguzi kuhusu madai ya ukiukaji wa kanuni za usajili yanayohusishwa na klabu hiyo wakati wa kukamilisha dili la mchezaji huyo.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *