WAKENYA WENGI BADO HAWAMUDU LISHE BORA
Ripoti ya Shirika la Chakula na Kilimo Duniani (FAO) inaonyesha kuwa takribani asilimia 66.6 ya Waafrika hawakuweza kumudu lishe bora mwaka 2025, licha ya kupungua kwa mfumuko wa bei katika mataifa mengi.
Ripoti hiyo imebainisha kuwa nchini Kenya, gharama ya vyakula vyenye virutubisho kama matunda, mboga, maziwa, mayai na protini za wanyama bado ni ya juu, hali inayowafanya mamilioni ya wananchi kushindwa kupata lishe bora.
FAO imeonya kuwa, ingawa bei ya baadhi ya vyakula vya msingi imepungua ikilinganishwa na kipindi cha mgogoro wa chakula wa mwaka 2022 hadi 2023, upatikanaji wa lishe bora bado ni changamoto kubwa kwa wananchi wengi nchini na katika ukanda wa Afrika Mashariki.
Imetayarishwa na Maurine Amwayi
English 































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































