#Local News

NTSA YAWAKAMATA WATU 45 KWA KOSA LA KUTOTUMIA KIVUKIO KATIKA ENEO LA NYAYO

Mamlaka ya Kitaifa ya Uchukuzi na Usalama Barabarani NTSA imewakamata watu 45 kwa kuvuka barabara badala ya kutumia kivukio cha daraja katika eneo la Uwanja wa Nyayo jijini  Nairobi.

NTSA imesema kuwa watu hao watashtakiwa kwa mujibu wa Sheria ya Trafiki  kwa kuvuka barabara katika maeneo yasiyoruhusiwa.

Mamlaka hiyo imeeleza kuwa operesheni hiyo ni sehemu ya juhudi za kuimarisha usalama barabarani na kupunguza idadi ya vifo vya watu wanaotembea kwa miguu.

Imetayarishwa na Hilda Ajema

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *