#Football #Sports

INGAVI ALENGA MAKOMBE NA SHABANA

Mshambuliaji wa zamani wa timu ya Taifa ya vijana wasiozidi miaka 17, Luis Ingavi, amesema lengo lake ni kuisaidia Shabana kutwaa mataji na si kushinda mechi pekee baada ya kujiunga na klabu hiyo kwa ajili ya msimu wa 2026/27.

Ingavi amesema anatamani kufunga zaidi ya mabao 10 katika msimu wake wa kwanza na kuchangia timu kupata ushindi mwingi ili iweze kushindania mataji.

Akizungumza baada ya kutambulishwa rasmi, mshambuliaji huyo amesema mashabiki wa Shabana, mazingira ya klabu, benchi la ufundi na mfumo wa uchezaji ndio vilivyomshawishi kujiunga na timu hiyo ya mjini Kisii.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *