#Local News

SERIKALI YAZINDUA MFUMO WA KIDIJITALI KUSHUGHULIKIA UHALIFU KWENYE VITUO VYA POLISI

Waziri wa Usalama wa Ndani Kipchumba Murkomen ametangaza kuwa serikali itasitisha matumizi ya mfumo wa jadi wa polisi uliokuwa ukitegemea taratibu za mwongozo na ushahidi wa kawaida, na badala yake kuanza kutumia Mfumo wa kidijitali wa biometriki.

Akizungumza katika makao makuu ya Idara ya Upelelezi wa kesi za  Jinai DCI, Murkomen amesema mfumo huo utaongeza uwezo wa utoaji huduma kwa wananchi.

Aidha, amesema mfumo huo utaboresha usajili wa watuhumiwa na utunzaji wa kumbukumbu za uhalifu kwa njia ya kidijitali, hatua ambayo itarahisisha ufuatiliaji na utambuzi wa wahalifu .

Imetayarishwa na Hilda Ajema

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *