#Local News

WATU 5 WAFARIKI BAADA YA KUPOROMOKEWA NA MGODI TRANSMARA

Watu watano wamethibitishwa kufariki dunia baada ya mgodi kuporomoka katika eneo la Lolgorian, Transmara Kusini, Kaunti ya Narok.

Naibu Kamishna wa Kaunti Ndogo hiyo ya Transmara Stephen Odeke, amesema juhudi za uokoaji bado zinaendelea, licha ya kutatizika kutokana na ukosefu wa vifaa maalumu vinavyohitajika .

Kulingana na Odeke idadi kamili ya wachimbaji waliokwama chini ya mgodi huo bado haijafahamika, huku ikiaminika kuwa watu kadhaa bado wamenaswa ndani ya mgodi huo.

Imetayarishwa na Hilda Ajema

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *