DUALE: HAKUNA WAGENI WALIOWEKWA KARANTINI LAIKIPIA
Waziri wa Afya Aden Duale amekanusha taarifa kwamba wahudumu saba wa misaada kutoka Marekani wamewekwa karantini katika kituo cha Ebola kinachofadhiliwa na Marekani katika Kituo cha Jeshi la Anga cha Laikipia.
Duale amesema serikali ilisimamisha ujenzi wa kituo hicho baada ya mahakama kutoa amri ya kusitisha mradi huo, hivyo taarifa hizo si za kweli.
Aidha, amesema serikali haitafichua maeneo ya vituo vya karantini na kutenga wagonjwa wa Ebola, akieleza kuwa kufanya hivyo kunaweza kuwakatisha tamaa wananchi kutafuta huduma za matibabu wanapohitaji.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 







































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































