#Football #Sports

KOCHA ABDALLAH JUMA AFARIKI DUNIA

Sekta ya soka nchini imepoteza mmoja wa makocha wake wenye uzoefu baada ya Abdallah Juma kufariki dunia kufuatia kuugua kisukari na saratani ya kongosho kwa muda mrefu.

Familia yake imethibitisha kuwa Juma alifariki saa saba usiku wa kuamkia Ijumaa, na anatarajiwa kuzikwa baadaye leo mjini Murang’a kwa mujibu wa taratibu za dini ya Kiislamu.

Katika kipindi cha zaidi ya miongo miwili ya ukocha, Juma alifundisha klabu kadhaa zikiwemo Thika United, KCB, Bidco United, Chemelil Sugar, Western Stima, FC Talanta, Vihiga Bullets na Murang’a SEAL, huku pia akiwahi kuwa kocha msaidizi wa AFC Leopards.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *