#Local News

WANAWAKE BUDALANG’I WAKUMBATIA BIASHARA ZA UVUAJI SAMAKI

Licha ya shughuli za uvuvi na ufugaji wa samaki kwa muda mrefu kuonekana kama kazi ya wanaume, wanawake katika eneo bunge la Budalangi, Kaunti ya Busia, wameanza kujitokeza na kuwekeza katika sekta hiyo katika Ziwa Victoria.

Wanawake hao wanasema wameingia katika biashara ya uvuvi na ufugaji wa samaki ili kujiongezea kipato, kuboresha maisha ya familia zao na kujipatia uwezo wa kujitegemea kiuchumi.

Kulingana na wanawake hao hatua hiyo imeanza kubadili mtazamo wa jamii kuhusu nafasi yao katika sekta ya uvuvi, huku ikitoa fursa zaidi za ajira na kuongeza ushiriki wao katika shughuli za uzalishaji wa chakula na maendeleo ya uchumi wa eneo hilo.

Imetayarishwa na Hilda Ajema

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *