MARTHA KOOME AMFUTA KAZI HAKIMU MMOJA KWA TUHUMA ZA HONGO
Jaji mkuu martha koome amemsimamisha kazi hakimu mmoja baada ya kukamatwa na tume ya maadili na kukabiliana na ufisadi EACC,kwa tuhuma za kupokea na kuomba hongo kuhusiana na kesi iliyokuwa mahakamani.
EACC inasema hakimu huyo pamoja na afisa wa uangalizi walikamatwa wakipokea hongo ya shilingi elfu 150 ili kuhakikisha mshtakiwa anapata adhabu isiyo ya kifungo.
Jaji koome amesema idara ya mahakama ina sera ya kutovumilia ufisadi huku taratibu za kinidhamu zikianza mara moja.
Imetayarishwa na Hilda Ajema
English 































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































