KINDIKI APUUZA MATOKEO YA UCHAGUZI WA OL KALOU
Naibu Rais Profesa Kithure Kindiki ameongoza viongozi wa Kenya Kwanza kupuuza ushindi wa upinzani katika uchaguzi mdogo wa ubunge wa Ol Kalou, akisema matokeo hayo hayana athari kwa maandalizi ya uchaguzi mkuu ujao.
Akizungumza mjini Embu Kindiki amesema Rais William Ruto bado yuko katika nafasi nzuri ya kutetea kiti chake na kupata muhula mwingine wa uongozi.
Aidha, amewataka viongozi wa eneo la Mlima Kenya kuendelea kushirikiana na kudumisha umoja, akisisitiza kuwa mshikamano utachangia maendeleo ya eneo hilo na taifa kwa ujumla.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 



















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































