#Local News

OBADO NA WASHTAKIWA WENZAKE KUSUBIRI HUKUMU HII LEO

Aliyekuwa Gavana wa Migori, Okoth Obado, pamoja na washtakiwa wenzake wawili, wanatarajiwa kufahamu hii leo iwapo watapatikana na hatia au wataachiliwa katika kesi ya mauaji ya mwanafunzi wa chuo kikuu Sharon Otieno na mtoto wake ambaye alikuwa hajazaliwa.

Mahakama Kuu katika Mahakama za Milimani itatoa hukumu dhidi ya Obado, aliyekuwa msaidizi wake Michael Oyamo na aliyekuwa Karani wa Kaunti ya Migori Caspal Obiero, takriban miaka minane baada ya kufunguliwa mashtaka ya mauaji mwaka 2018.

Shirikisho la Wanasheria Wanawake nchini (FIDA-Kenya), ambalo limekuwa likifuatilia kesi hiyo kwa niaba ya familia ya Sharon, limesema lina matumaini kuwa hukumu ya mahakama itaongozwa na ushahidi uliowasilishwa wakati wa kusikilizwa kwa kesi pamoja na matakwa ya sheria.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *