#Football #Sports

ODEMBA ASIFU HATUA YA NEKESA ULAYA

Kocha wa Harambee Starlets, Beldine Odemba, amesema uhamisho wa mshambuliaji Valarie Nekesa kwenda klabu ya CD Tenerife Femenino nchini Hispania unaonyesha mafanikio ya mfumo wa soka la shule nchini katika kukuza vipaji.

Nekesa mwenye umri wa miaka 18 alitambulishwa rasmi na klabu hiyo tarehe 11 Julai, na kuwa Mkenya wa tatu kusajiliwa na klabu ya nchini Hispania baada ya Cynthia Shilwatso na Vivian Corazon Aquino.

Odemba amesema hatua ya Nekesa inapaswa kuhamasisha uwekezaji zaidi katika ukuzaji wa vipaji vya soka mashinani, huku Harambee Starlets ikiendelea na kambi ya mazoezi kujiandaa kwa Kombe la Mataifa ya Afrika kwa Wanawake (WAFCON) 2026 nchini Morocco.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *