#Local News

HAKIMU WA KANGEMA ASIMAMISHWA KAZI KWA MADAI YA HONGO

Hakimu wa mahakama ya Kangema, Martin Kinyua, amesimamishwa kutekeleza majukumu yake ya kimahakama baada ya kukamatwa na Tume ya Maadili na Kupambana na Ufisadi (EACC) kwa tuhuma za kuomba na kupokea hongo.

Kinyua alikamatwa pamoja na Julius Irungu, huku wawili hao wakidaiwa kuomba shilingi 170,000 kutoka kwa mfanyabiashara wa Murang’a aliyekuwa amepatikana na hatia ya kupata fedha kwa njia ya udanganyifu, wakiahidi kumpatia adhabu isiyohusisha kifungo.

EACC imesema imepanua uchunguzi kuhusu mienendo ya baadhi ya maafisa wa mahakama kufuatia ongezeko la malalamiko kutoka kwa wananchi kuhusu madai ya ufisadi katika mfumo wa utoaji haki.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *