NYAMITA: USHINDI WA OL KALOU SIO KIPIMO CHA URAIS
Mbunge wa Uriri, Mark Nyamita, amesema upinzani unasherehekea ushindi wa uchaguzi mdogo wa Ol Kalou kupita kiasi, akidai kuwa ni ushindi mmoja tu ambao hauwezi kuamua mwelekeo wa siasa za kitaifa.
Nyamita amesema uchaguzi huo umeonyesha kuwa hakuna muungano wa kweli wa upinzani, akieleza kuwa vyama vya upinzani vilishindwa kusimamisha mgombea mmoja kama ishara ya umoja wao.
Aidha, amesisitiza kuwa matokeo ya Ol Kalou hayana uhusiano na uchaguzi wa urais, akibainisha kuwa Rais William Ruto hakuwa mgombea katika uchaguzi huo.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































