ORERO ATAKA HATUA KALI DHIDI YA WAHUNI
Mbunge wa Kibra Peter Orero amemtaka Inspekta Jenerali wa Polisi Douglas Kanja kuchukua hatua madhubuti kukabiliana na ongezeko la vitendo vya uhuni vinavyoshuhudiwa katika shughuli za kisiasa.
Mbunge huyo pia amewataka wanasiasa kuacha kutumia wahuni kutekeleza malengo yao ya kisiasa, akisema tabia hiyo inachochea vurugu na kuhatarisha usalama wa wananchi.
Aidha, ameonya kuwa ikiwa hatua za haraka hazitachukuliwa, nchi inaweza kuelekea katika hali ya kutotii sheria, hasa wakati taifa linapojiandaa kwa uchaguzi mkuu ujao.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































