#Rugby #Sports

RAGA: KABRAS NA KCB KUFUNGUA MSIMU KWA DABI

Mabingwa watetezi wa Kombe la Kenya, Kabras Sugar, wataanza kampeni ya msimu wa 2026/2027 kwa mechi kali dhidi ya mahasimu wao KCB mwezi Novemba katika uwanja wa Kakamega Showground.

Tofauti na misimu iliyopita ambapo timu hizo zilikutana mwishoni mwa msimu, safari hii zitavaana katika mchezo wa ufunguzi huku KCB ikisaka kulipiza kisasi baada ya kupoteza fainali ya mwaka 2026 kwa mabao 14-8.

KCB haijaionja ushindi dhidi ya Kabras tangu ilipoibuka na ushindi wa 28-20 mwezi Februari mwaka 2022, jambo linaloongeza ushindani wa pambano hilo linalosubiriwa kwa hamu

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *