ALIYEKUWA KAMISHNA WA IEBC MOHAMMED SHARAWE AMEAGA DUNIA
Aliyekuwa kamishna wa tume ya uchaguzi na mipaka nchini IEBC Mohammed Abdulahi Sharawe ameaga dunia.
Kulingana na familia yake Mohamed ameaga dunia usiku wa kuamkia leo, Sharawe aliwahi kuwa katibu wa idara ya bara bara na kazi za umma wakati wa utawala wa hayati Rais Daniel Arap Moi kabla ya kuhudumu kwenye wizara ya utafiti mafunzo ya ufundi na Technolojia.
Sharawe aidha alichaguliwa kuwa kamishna wa IEBC baada ya kupitishwa kwa katiba mpya mwaka wa 2010 na kuhusika katika chaguzi kati yam waka wa 2011 hadi 2016.
Imetayarishwa na Hilda Ajema
English 







































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































