#Business

BIASHARA CHANGA NCHINI ZADIDIMIA KATIKA NUSU YA KWANZA MWAKANI

Ni hasara kwa kampuni zinazoanza na zile changa nchini kwani zimepata ufadhili wa Shilingi bilioni 16.3 katika nusu ya kwanza ya mwaka 2026, kiasi ambacho ni kidogo ikilinganishwa na Shilingi bilioni 17 zilizopatikana katika kipindi kama hicho mwaka uliopita.

Ripoti hiyo inaonyesha kuwa Kenya inashika nafasi ya tatu barani Afrika kwa upande wa ufadhili wa kampuni changa, ikifuatia Misri iliyovutia Shilingi bilioni 42.3 na Nigeria iliyopata Shilingi bilioni 32.8.

Ikizingatiwa ufadhili wa hisa pekee, Nigeria imeongoza kwa dola milioni 214, ikifuatiwa na Misri kwa dola milioni 183, huku Afrika Kusini ikipata dola milioni 66 na Kenya dola milioni 46. Mbali na masoko manne makubwa zaidi ya kampuni changa barani, Tanzania, Côte d’Ivoire na Morocco kila moja imevutia ufadhili wa zaidi ya dola milioni 25 katika miezi sita ya kwanza ya mwaka.

Imetayarishwa na Maurine Amwayi

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *