#International

BOBI WINE AIBUA WASIWASI KUHUSU MBUNGE ANAYEDAIWA KUTOWEKA

Kiongozi wa upinzani nchini Uganda, Bobi Wine, ameibua wasiwasi kuhusu aliko Mbunge wa upinzani Muwanga Kivumbi, akidai kuwa hajulikani alipo kwa siku kumi baada ya kudaiwa kutekwa.

Kupitia ujumbe aliouchapisha kwenye mtandao wa X, Bobi Wine amesema amepokea taarifa zinazodai kuwa Kivumbi aliteswa katika kambi ya kijeshi ya Kasenyi Special Forces Command (SFC) na anazuiliwa mbali na umma.

Bobi Wine ametoa wito kwa mamlaka kuchunguza madai hayo na kueleza aliko mbunge huyo, akisema kumekuwa na visa vya awali ambapo viongozi wa upinzani walidaiwa kuzuiliwa bila kufikishwa hadharani.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *