KARUA AKATAA NAFASI YA NAIBU RAIS
Kiongozi wa chama cha People’s Liberation Party Martha Karua, amesema hatakubali kugombea nafasi ya Naibu Rais chini ya muungano wa upinzani, akisisitiza kuwa atalenga urais au kumuunga mkono atakayeteuliwa kupeperusha bendera ya muungano huo.
Akizungumza katika mahojiano na kituo kimoja cha runinga, Karua amesema viongozi wa upinzani wamekubaliana kupata mgombea mmoja wa urais kupitia mchakato wa uteuzi utakaozingatia sheria na makubaliano ya muungano.
Aidha, Karua pia ameangazia mageuzi ambayo atayafanya iwapo atachaguliwa kama rais.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































