HINGA AKANUSHA MADAI YA UONDOAJI WA FEDHA ZA BOMA YANGU
Katibu Mkuu wa Idara ya Makaazi na Ustawi wa Miji, Charles Hinga, amekanusha madai kuwa Wakenya wameondoa shilingi bilioni 2.56 kutoka kwenye jukwaa la akiba la nyumba nafuu la Boma Yangu.
Hinga amesema taarifa zinazosambazwa kupitia vyombo vya habari na mitandao ya kijamii si sahihi na hazielezi hali halisi ya utekelezaji wa mpango huo wa nyumba za bei nafuu.
Amefafanua kuwa zaidi ya theluthi mbili ya fedha zinazotajwa zilitumika kama amana ya ununuzi wa nyumba mpya katika miradi mbalimbali, isipokuwa ule wa Park Road, na si fedha zilizotolewa na wanachama kama inavyodaiwa.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































