KAMATI YA NHIF YAZINDULIWA KUCHUNGUZA MADENI
Ni afuueni kwa taasisi za afya ambazo zilitoa huduma za afya chini ya bima ya afya ya awali NHIF baada ya Wizara ya Afya kuzindua Kamati ya Uthibitishaji wa Madeni ya Matibabu ya NHIF iliyoanzishwa tarehe 30 Machi.
Kamati hiyo inachunguza madeni ya NHIF yaliyobaki kutoka Julai 2022 hadi Septemba 2024 na kutoa mapendekezo kuhusu ulipaji wake.
Kamati, inayotarajiwa kuhudumu kwa miezi mitatu, itahakikisha kugundua madai ya udanganyifu na kupendekeza hatua na mageuzi kwa serikali ili kuzuia kurudiwa kwa madai yasiyothibitishwa.
Imetayarishwa na Janice Marete
English 































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































