KIBWAGE AITWA KWNYE KIKOSI CHA HARAMBEE STARS
Beki wa Tusker FC anayetatizika, Michael Kibwage ana furaha baada ya kujumuishwa katika kikosi cha muda cha kocha Benni McCarthy cha wachezaji 30 kwa ajili ya Michuano ya Mataifa ya Afrika (CHAN).
Kibwage amekuwa na msimu mgumu, baada ya kukosekana kwa miezi miwili kwenye mzunguko wa pili wa ligi kuu kutokana na jeraha la paja na kulazimika kufanya bidii kurejea kikosi cha kwanza. Alikuwa na kipindi kizuri kwenye mzunguko wa kwanza kabla ya jeraha kumtoa Desemba.
Kibwage ametaja kuitwa kwake kama uhai mpya na kutumai kuwa kitamtia moyo kabla ya msimu mpya.
Beki huyo wa kati amewahi kuichezea timu ya taifa na pia kuwa nahodha wa timu ya Kenya ya vijana chini ya umri wa miaka 23 wakati fulani.
Hata hivyo, kutoshiriki soka kwa mwaka mmoja na nusu kulimfanya afifie taratibu, lakini kwa misimu miwili iliyopita, amefanikiwa kujinyanyua upya.
Kikosi cha Harambee Stars kwa ajili ya CHAN kinaingia kambi ya makazi hapo kesho.
Imetayarishwa na Nelson Andati
English 































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































