GACHAGUA: MIMI NDIYE KIGOGO WA UPINZANI
Aliyekuwa naibu Rais Rigathi Gachagua ametanagaza kuwa ndiye yuko katika nafasi nzuri ya kuwa kigogo wa upinzani na kumenyana na Rais William Ruto kwenye uchaguzi mkuu ujao.
Akizungumza katika jimbo la Boston nchini Marekani, Gachagua amesema ana uwezo wa kumfanya Rais Ruto kutochaguliwa kwa muhula wa pili.
Aidha, amefichua kuwa upinzani utaweka wazi atakayepeperusha bendera ya urais mwezi Disemba mwaka ujao.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































