FAMILIA MURANG’A YALILIA HAKI
Familia moja katika kaunti ya Murang’a inalilia haki baada ya mwanao kudaiwa kukanyagwa na gari la kampuni moja ya ulinzi na kusababisha kifo chake.
Kamanda wa polisi eneo la Murang’a Kusini Hassan Bashir, amesema mwendazake Michael Murigi alikuwa na mwenzake wakisafiri kwa piki piki kabla ya kugongwa upande wa nyuma.
Piki piki hiyo pamoja na gari lililohusika zimefanyiwa uchunguzi na maafisa wa mamlaka ya usalama barabarani NTSA.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































