ALIYEKUWA CHIFU WA EASTLEIGH KASKAZINI AHUKUMIWA
Mahakama ya rufaa jijini nairobi imeidhinisha hukumu ya aliyekuwa chifu wa Eastleigh kaskazini ,Paul Kuria kwa madai ya kupokea hongo kutoka kwa mkaazi mmoja akitaka stakabadhi za uraia kwa jamaa zake.
Katika utetezi wake, ngugi amedai kuwa alikamatwa na maafisa wa tume ya maadili na kupambana na ufisadi eacc, akisema kwamba kukamatwa kwake kulichochewa kisiasa.
Mahakama ya rufaa ilitupilia mbali rufaa hiyo kwa ujumla wake, na kuthibitisha hukumu dhidi ya chifu huyo wa zamani.
Imetayarishwa na Jones Koikai
English 































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































