POLISI ‘WAHALIFU’ WAKAMATWA
Maafisa wa DCI wanatarajiwa kuwafikisha mahakamani hii leo washukiwa 4 wakiwemo maafisa wa zamani na wa sasa wa polisi wanaohusishwa na visa vya utekaji nyara na wizi wa kimabavu jijini Nairobi.
Mmoja wa washukiwa Cleophas Wambua aliyekuwa akihudumu kama afisa wa polisi katika kaunti ya Homa Bay, alinaswa hapo jana mafichoni eneo la Kitengela akiwa na mwenzake James Omwami.
Wengine ni maafisa wa DCI Kipkurui Bii na Mwalim Said Mwalole, huku waathiriwa wakieleza kuhangaishwa na washukiwa hao.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































