#Local News

RUTO ATANGAZA SERA YA KUWALINDA “WACHACHE”

Kenya imejiunga na ulimwengu kuadhimisha siku ya jamii za watu wachache, rais William Ruto akitangaza kuidhinishwa kwa sera itakayotetea haki za jamii hizo.

Akizungumza kwenye kikao na jamii hizo kinacheoendelea katika Ikulu ya Nairobi, Ruto ameahidi kuwa sera hiyo iliyoidhinishwa na baraza la mawaziri, itafanikisha vita dhidi ya dhuluma dhidi ya jamii hizo ikiwemo umiliki wa mashamba na nafasi za ajira katika ngazi zote za serikali.

Sera hiyo itahitaji mkono wa bunge kabla ya kuwa sheria.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *