#International

KIRITIMATI YAKARIBISHA 2026!

Kisiwa cha Kiritimati yaani Christmas islands kimekuwa sehemu ya kwanza ya ulimwengu kuukaribisha mwaka mpya wa 2026.

Kisiwa hicho kilichoko katika taifa la Kiribati katika bahari ya Pacific kusini mwa Hawaii na kaskazini mashariki mwa taifa la Australia, kilipata uhuru wake kutoka taifa la Uingereza mwaka 1979, na kina takribani wakazi 116.

New Zealand imekuwa ya pili kuukaribisha mwaka mpya, huku visiwa vya Baker na Howland vilivyo eneo la kati la bahari ya Pacific vikiratibiwa kuwa sehemu ya mwisho ya ulimwengu kuukaribisha mwaka mpya. 

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

Test rest

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *