WANAFUNZI NAROK NJIA PANDA
Ufunguzi wa shule umeingia siku ya 3 hii leo huku wanafunzi kadhaa katika eneo la Ang’ata Barrikoi kaunti ya Narok wakikosa kurejea shuleni kuhusiana na hofu ya usalama kufuatia mapigano baina ya jamii za eneo hilo.
Baadhi ya shule eneo hilo zimesalia kuwa mahame, huku nyingine kama vile ile ya Siteti zikitumika kama hifadhi ya wakimbizi wa mapigano hayo.
Wakazi wameitaka serikali kuimarisha operesheni ili kurejesha utulivu, huku KUPPET ikiwaonya wanachama wake dhidi ya kurejea katika shule za eneo hilo.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 






























































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































