MIGAWANYIKO YA KISIASA YAIBUKA
Tofauti za kisiasa zimeendelea kuibuka miongoni mwa vyama tanzu vya muungano wa upinzani na Kenya Kwanza, baadhi ya viongozi wakitangaza kugura vyama hivyo na kujiunga na vyama vinavyoegemea serikali ya Kenya Kwanza.
Wa hivi punde ni naibu kinara wa chama cha DAP-K na naibu gavana wa Kakamega Ayub Savula, ambaye amegura chama hicho na kutangaza kuingia serikalini.
Haya yanajiri huku naibu kinara wa chama cha Ford Kenya na gavana wa Bungoma Ken Lusaka, akiteuliwa na Rais William Ruto kama mratibu wa kampeni za Ruto eneo la Magharibi kwenye uchaguzi mkuu ujao.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 






























































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































