#Football #Sports

GUARDIOLA APOTEZA TUMAINI EPL

Kocha mkuu wa Manchester City Pep Guardiola amekiri kuwa klabu hiyo haiwezi kufikiria kuipata Arsenal kileleni mwa ligi katika kinyanga’nyiro cha kusaka ubingwa wa ligi hiyo msimu huu baada ya msururu wao wa sare kufikia mechi 3 mfululizo.

Licha ya Erling Haaland kuwaweka City kifua mbele kakatika kipindi cha kwanza jinsi ilivyofanyika dhidi ya Chelsea, Manchester walipoteza pointi 2 muhimu baada ya kuruhusu Kaoru Mitoma kuwafungia Brighton bao katika dakika ya 60 na kulazimisha sare ya bao 1-1.

Haaland ambaye alifunga bao lake la 150 na la 35,000 la ligi kuu ya EPL tangu kuanzishwa kwake mwaka 1992, alipoteza nafasi nyingine nyingi ambazo zingewapa ushindi bila matatizo na kuipa Arsenal shinikizo.

Akizungumza baada ya mechi hiyo, Guardiola amelalamikia nafasi zilizobuniwa ila zikakosa kumaliziwa, na kuwaacha vijana wake wakiwa pointi 5 nyuma ya the Gunners ambao huenda wakaongeza mwanya hadi pointi 8 iwapo watavuna ushindi dhidi ya Liverpool leo usiku.

City wanalenga kuimarisha mashambulizi yake kwa kumsajili raia wa Ghana Antoine Semenyo kutoka Bournemouth, ila wangali wanavuja kwenye safu ya ulinzi hasa kutokana na majeraha kwa mabeki wa kati Reuben Diaz na Josko Gvardio.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

GUARDIOLA APOTEZA TUMAINI EPL

LEOPARDS WAREJEA UONGOZINI KPL

GUARDIOLA APOTEZA TUMAINI EPL

SESKO ATALETA MWANGA, FLETCHER

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *