KNEC: THIBITISHA USAJILI WA MWANAO
Baraza la mitihani ya kitaifa KNEC limewataka wazazi kuthibitisha kwamba wanao wamesajiliwa kwenye mitihani ya kitaifa ya gredi ya 6, 8 na kidato cha 4 kwa kutumia mfumo wa ujumbe mfupi wa maandishi SMS utakaotumika kuanzia Aprili mwaka huu.
Afisa mkuu mtendaji wa KNEC David Njeng’ere, amesema hilo litapunguza changamoto za watahiniwa kukosa kukalia mitihani yao dakika za mwisho.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































