#Football #Sports

MABAO YA SEMENYO, CHERKI YAWAPA CITY USUKANI

Manchester City walitia guu moja ndani ya fainali za Carabao Cup jana usiku, kufuatia mabao ya sajili mpya Antoine Semenyo na Rayan Cherki yaliyowapa ushindi wa mabao 2-0 ugenini dhidi ya bingwa mtetezi Newcastle United.

Semenyo aliyewasili wiki jana kutoka Bournemouth kwa kima cha pauni milioni 65, ameonyesha ubabe wake, akiwa amefunga mara 2 na kuchagia bao 1 kwenye mechi 2 za mwanzo.

Mkondo wa pili wa nusu fainali hiyo itachezwa tarehe 4 mwezi ujao ugani Etihad Statdium, mshindi akikata tiketi ya kuingia Wembley kwa fainali dhidi ya timu bora kati ya Arsenal na Chelsea.

Wawili hao watamenyana leo usiku kwenye debi la London katika mkondo wa kwanza katika uwanja wa Stamford Bridge, kabla ya marudiano tarehe 3 mwezi ujao uwanjani Fly Emirates.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

MABAO YA SEMENYO, CHERKI YAWAPA CITY USUKANI

AFCON 2025: USIKU WA NUSU FAINALI

MABAO YA SEMENYO, CHERKI YAWAPA CITY USUKANI

CARRICK ATEULIWA KUINOA UNITED

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *