AKONNOR AIPONGEZA GOR MAHIA BAADA YA KUICHAPA MARA SUGAR
Kocha mkuu wa Gor Mahia Charles Akonnor amewapongeza wachezaji wake kufuatia ushindi wa mabao 3–0 dhidi ya Mara Sugar katika mechi ya Ligi Kuu ya FKF iliyochezwa Jumapili Januari 18, 2026, katika uwanja wa Nyayo National Stadium.
Akizungumza baada ya mechi hiyo, Akonnor alisema alifurahishwa na utulivu na maamuzi sahihi ya wachezaji wake uwanjani, akibainisha kuwa walitekeleza mpango wa mchezo ipasavyo.
Ushindi huo umeiwezesha Gor Mahia kupanda kileleni mwa msimamo wa ligi kwa pointi 33, sawa na wapinzani wao wa jadi AFC Leopards, lakini K’Ogalo wakiwa mbele kwa ubora wa magoli.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































