USIKU MUHIMU KWA KLABU ZA UEFA
Mechi ya 7 kati ya 8 ya awamu ya kwanza ya ligi ya klabu bingwa barani Ulaya, UEFA, zitachezwa usiku wa leo ambapo timu kadhaa ikiwemo Liverpool, Real Madrid na Inter Milan zitalenga kupata ushindi ili kujihakikishia kufuzu moja kwa moja katika awamu ya 16 bora kutokana na kudidimia kwa matumaini ya kupata mataji ya nyumbani msimu huu.
Licha ya kuiongoza Liverpool kucheza mechi 12 bila kupoteza hadi sasa, kocha Arne Slot atakuwa na kibarua ca kuhakikisha klabu yake inafanya vyema Ulaya, ikizingatiwa kuwa inakabiliwa na mlima kutetea taji la EPL.
Tayari timu za Arsenal, bingwa mtetezi PSG, Manchester City na Atalanta zimejihakikishia nafasi katika awamu ya mwondoano, na zitahakikisha kumaliza katika nafasi ya 8 bora ili kufuzu awamu ya 16 bora bila kupitia mwondoano.
Viongozi wa Serie A, Inter Milan, watalenga kuweka nyuma kichapo dhidi ya Liverpool kwenye mechi yao iliyopita, watakapomenyana na timu ya pekee ambayo imeandikisha ushindi katika mecho zote 6 za mwanzo, Arsenal.
Hata hivyo, vijana hao wa Christian Chivu watakabiliwa na ushindani mkali nyumbani, ikizingatiwa kuwa Arsenal wanalenga kupata nafasi katika raundi ya 16 kabla ya mechi ya mwisho kutokana na mrundiko wa mechi.
Inter wameinyorosha Arsenal katika mechi 3 kati ya 4 zilizopita za ubingwa huo.
Wakati uo huo, mkufunzi mpya wa Real Madrid Alvaro Arbeola atalenga kuendeleza ushindi wa klabu hiyo baada ya kuandikisha ushinddi dhidi ya Levante kwenye La Liga, atakapomenyana na Monaco.
Wachezaji wake wakuu akiwemo Vinicius junior na Jude Bellingham, kwa sasa wanapitia kipindi kigumu baada ya kuzomewa na mashabiki wao.
Miamba wengine wa kuangaziwa ni Barcelona yake Hansi Flick, ambao msururu wa mechi 11 bila kupoteza uliishia kwenye kichapo cha mabao 2-1 dhidi ya Real Sociedad wikendi.
Barca waliofika awamu ya nusu fainali ya UEFA msimu jana, wamo katika nafasi ya 15 kwa pointi 10, na Flick atalenga kuweka kando masaibu ya wikendi atakapovaana na Slavia Parague.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































