RUTO AAGIZA HATIMILIKI YA SOKO LA GIKOMBA
Rais William Ruto ameagiza hatimiliki ya Soko la Gikomba jijini Nairobi kutolewa ndani ya siku 90 akisema soko hilo liko kwenye ardhi ya umma na kwamba kutoa hatimiliki kwa jina la Kaunti ya Nairobi kutatatua suala la umiliki wake mara moja
Akitoa kauli hiyo wakati wa mkutano na wafanyabiashara wa Soko la Gikomba uliofanyika katika Ikulu ya Nairobi, Ruto amewaagiza Waziri wa Ardhi, Alice Wahome, na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Nixon Korir, kushirikiana na Tume ya Kitaifa ya Ardhi ili kuhakikisha hatimiliki hiyo inatolewa.
Aidha, Rais Ruto ametangaza kuwa ujenzi wa awamu ya tatu ya Soko la Gikomba utaanza baada ya kukamilika kwa awamu ya pili.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































