#Local News

VIFO VYA ZAIDI YA 290 VIMERIPOTIWA JANUARI 2026, TAKWIMU ZA POLISI

Zaidi ya watu 290 wamefariki katika siku 21 za mwanzo wa Januari 2026, kulingana na takwimu zilizokusanywa na polisi.

Hapo jana watu saba waliuawa katika ajali tofauti nchini, na kuongeza idadi ya vifo hadi 294 katika siku 21 miongoni mwao wakiwa ni Pamoja na watembea miguu wawili, abiria wawili, waendesha pikipiki wawili, na abiria wa pikipiki mmoja.

Polisi wamesema wengine saba walijeruhiwa vibaya, wakiwemo waendesha pikipiki wanne, mtembea miguu mmoja, na dereva mmoja.

Hii inaashiria ongezeko la watu 18 ikilinganishwa na vifo 276 vilivyorekodiwa katika kipindi hicho hicho mwaka 2025.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *