BABU AMUUNGA MKONO AMOS WANJALA KUNG’ARA VALENCIA
Kocha wa Rising Stars Salim Babu amempa imani beki Amos Wanjala
kuonyesha uwezo wake katika klabu yake mpya ya Valencia CF.
Nahodha wa timu ya taifa ya Kenya chini ya umri wa miaka 20
amejiunga na kikosi cha akiba cha miamba hao wa Uhispania siku ya
Jumamosi, hatua iliyohitimisha safari yake ya miezi 15 na klabu ya
Athletic Club Torrellano ya daraja la tano.
Babu amesema Wanjala ana vipaji na nidhamu ya kutosha kumsaidia
kupanda ngazi hadi kikosi cha wakubwa cha Valencia siku zijazo.
Kocha huyo pia amepongeza uhamisho huo akisema ni fursa
itakayofungua milango kwa wachezaji wengine wa Kenya kupata
nafasi katika ligi za juu barani Ulaya.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































