VYAMA TANZU VYAPINGA MAGEUZI AZIMIO
Mvutano wa kisheria unanukia ndani ya muungano wa Azimio la Umoja One Kenya kuhusiana na mageuzi ya hivi punde kwenye uongozi wake, baada ya kundi la vyama wanachama kupinga mageuzi hayo likiyataja kuwa kinyume na sheria.
Likiongozwa na katibu mkuu wa chama cha National Liberal Party, NLP, Omondi Koyoo, kundi hilo limemwandikia msajili wa vyama vya kisiasa likimtaka asitekeleze mageuzi hayo, kwa misingi kwa yalifanya kisiri bila kushirikishwa kwa baadhi ya vyama wanachama.
Kwenye mageuzi hayo, kinara wa Wiper Kalonzo Musyoka aliteuliwa kuwa kinara mpya wa Azimio kufuatia kifo cha Raila Odinga, huku mbunge wa Suba North Caroli Omondi akichukua mahala pa Junet Mohammed kama katibu mkuu..
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































