WAMBUA: NIDHAMU YA MBINU NI MUHIMU KWA SHUJAA
Kocha mkuu wa Kenya Sevens, Kevin Wambua, amesema usimamizi mzuri wa mchezo na nidhamu ya mbinu ndiyo yatakuwa mambo muhimu yatakayoamua hatima ya Shujaa katika mashindano ya World Sevens Division Two yanayoanza wikendi hii katika Uwanja wa Nyayo.
Wambua amesema mashindano hayo ni makubwa zaidi kuwahi kuandaliwa nyumbani, huku fahari ya taifa na nafasi ya kupandishwa daraja vikiwa hatarini kwa timu ya Kenya.
Aidha Amesisitiza kuwa Shujaa lazima iwe makini katika kufanya maamuzi na kuwa kali katika utekelezaji wa mbinu ili kuhimili ushindani mkali unaotarajiwa katika mashindano ya siku mbili.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































