#Boxing #Sports

LIZ ANDIEGO AINGIA NGUMI ZA KULIPWA

Bondia wa kike mwenye mafanikio makubwa nchini, Liz Andiego, sasa amejiunga rasmi na ngumi za kulipwa, akifungua ukurasa mpya katika taaluma yake.

Bondia huyo mwenye umri wa miaka 37 atapanda ulingoni kwa mara ya kwanza kama mtaalamu Februari 27, 2026, jijini Nairobi, ambapo atamenyana na Chiku Iddi wa Tanzania katika pambano la raundi nne uzani wa kati wa juu, litakalofanyika katika jumba la Mass House kando ya Barabara ya Ngong.

Andiego ametia saini mkataba na kampuni ya Kalakoda Promotions, huku Shirikisho la Ngumi la Kenya likithibitisha kuidhinisha hatua hiyo na kuendelea kumhifadhi katika kikosi cha taifa.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

LIZ ANDIEGO AINGIA NGUMI ZA KULIPWA

WAMALWA AZUNGUMZIA VIFO KITENGELA

LIZ ANDIEGO AINGIA NGUMI ZA KULIPWA

AKONNOR ASIFU GOR MAHIA

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *