KMPDU YATOA MAKATAA COAST GENERAL
Serikali ya kaunti ya Mombasa ina siku 7 kuchukua hatua na kumrejesha kazini afisa mkuu mtendaji wa hospitali ya rufaa ya Coast General Daktari Iqbal Kandwalla la sivyo madkatari wasitishe huduma zao na kulemaza matibabu kwenye hostali hiyo.
Kandwalla alisimamishwa kazi kwa madai ya utepetevu kazini unaohusishwa na kifo cha Ali Kibwana hospitalini humo, aliyekuwa mlinzi wa usiku katika afisi ya mbunge wa Mvita Mohammed Machele.
KMPDU imepinga uamuzi wa kumsimamisha kazi, ikitaja kuwa kinyume na sheria.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































